Tuesday 19 March 2013

LWAKATARE APANDISHWA KIZIMBANI, ASOMEWA MASHITAKA YA UGAIDI

            MKUU wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare, leo amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam na kusomewa mashitaka manne ya ugaidi. Lwakatare amepandishwa kizimbanai sambamba na kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Ludovick Joseph. Katika kesi hiyo Lwakatare anatetewa na mawakili watano, Tundu Lissu, Profesa Safari, Nyaronyo Kicheere, Mabere Marando  na Peter Kibatara. 

No comments:

Post a Comment